Bw.Khamis J. Katimba
Mchumi wa Mji
Mkuu wa Idara ya Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
IDARA YA MIPANGO, TAKWIMU NA UFUATILIAJI
Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji ni moja kati ya Idara za Halmaashauri ya Mji wa Babati. Idara ina jumla ya watumishi 6 akiwemo Mkuu wa Idara, Wachumi 3, Mtakwimu mmoja pamoja na Katibu Muhtasi.
Majukumu makubwa ya Idara hii ni kama ifuatavyo:-
Kuratibu shughuli zote za maendeleo za Halmashauri.
Kutafsiri sheria, sera na miongozo ya kisekta.
Kuratibu zoezi la uandaaji mipango Mikakati ya maendeleo kwa kushirikiana na wadau wa nje na ndani ya Halmashauri.
Kuwezesha shughuli za kiuchumi na kijamii zinazofanyika Halmashauri.
Kutafuta, kuchambua na kutaafsiri takwimu za kiuchumi na kijamii.
Kuratibu shughuli za uwekezaji kwa kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya Halmashauri.
Kubuni mikakati mbalimbali ya kuongeza vyanzo vya mapato ya Halmashauri.
Kuandaa Bajeti ya Halmashauri na kuratibu utekelezaji wake.
Kufanya ufuatiliaji na tathimini wa shughuli za kiuchumi na kijamii.
Kuhimiza na kushirikisha jamii katika upangaji na utekelezaji wa miradi/program za maendeleo.
Katimba, Khamis J.
MCHUMI WA MJI
H/MJI BABATI
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati