Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amezindua rasmi Maonesho ya Biashara,Madini,Viwanda na Kilimo “ Tanzanite Manyara Trade Fair”, Mkoani Manyara,Maonesho hayo yameanza tarehe 20 hadi 30 Oktoba 2024, yenye kauli mbiu "Manyara kwa Ustawi wa Biashara na Uwekezaji.”
Mhe. Kigahe amewapongeza waandaaji na waratibu wa maonesho hayo TCCIA pamoja na Wadhamini wote amboa wamedhamini maonesho hayo akiwemo Mati superbrands na wengine.
Aidha Mhe.Kigahe amezitaka Taasisi za Umma kama vile TRA pamoja na Ofisi za biashara ngazi ya Mkoa na Halmashauri kuwasaidia wafanyabiashara kurasimisha biashara ili waweze kukua kibiashara na amesisitiza kuwa kila biashara inachangia mapato 40% kwa Serikali hivyo basi ili kuepuka kupoteza mapato hayo ni vyema watumie utaratibu stahiki katika kurasimisha biashara na sio kufunga na kunyang’anya leseni za biashara kwa wafanyabiashara.
Vilevile Mhe. Exaud ameeleza kuwa maendeleo ya kweli yanapatikana kwa kushirikiana Sekta binafsi na Serikali na ameongeza kuwa Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira ya wafanyabiashara kwa kuhuisha Sera ya Taifa ya Biashara na kuandaa mikakati mbalimbali ili kukuza na kuvutia Uwekezaji.
Pia Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Emmanuella Kaganda Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara amemkaribisha Mhe. Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara katika maonesho hayo na amesema kuwa maonesho hayo ni fursa ya kuutangaza Mkoa wa Manyara kitaliii kupitia hifadhi ya Tarangire, Ziwa Babati na Madini ya Tanzanite yanayopatikana nchini Tanzania pekee.
Aidha Afisa Biashara Halmashauri ya Mji Babati Bi. Upendo Edwin amewataka wafanyabiashara kutembelea banda la Halmashauri ya Mji wa Babati ili wapate elimu ya biashara,kupata leseni za biashara kwa njia ya mtandao na waweze kupata uelewa wa fursa za kibiashara zinazopatikana Mkoani Manyara.
Sambamba na hayo wafanyabiashara wamemshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufungua mipaka ya kibiashara ya nchi jirani za Afrika mashariki, Kenya ,Uganda,Rwanda na kuwezesha wafanyabiashara wa Tanzania kufanya biashara nchi jirani.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati