• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango Miji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi
      • Usafi na Mazingira
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Utoaji wa Leseni ya Biashara
    • Utoaji wa Leseni za Vileo
    • Utoaji wa Kibali cha Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

Mhe.Queen Sendiga ameweka jiwe la msingi katika shule ya mpya ya Awali na Msingi

Imechapishwa: September 15th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Mhe. Queen Cuthbert Sendiga akiwa katika ziara yake ameweka jiwe la msingi Shule ya Awali na Msingi Queen Cuthbert Sendiga  kata ya Maisaka Halmashauri ya Mji wa Babati. Ambapo shule hiyo ni mradi wa BOOST wa kuimarisha na kuboresha elimu ya Awali na Msingi.Mradi huu unatekelezwa nchini kwa muda miaka 5 hivyo kukamilika mwaka 2025/2026 na umelenga kunufaisha miundombinu ya elimu kwa madarasa ya Awali na Msingi.

Pia Mhe.Sendiga amepanda miti katika Shule mpya ya Queen Sendiga kwa lengo la kuimarisha mazingira na kufanya muonekano mzuri wa shule hiyo ya awali na Msingi.Pamoja na kukagua majengo ya ofisi,madarasa na vyoo vya shule hiyo. Amewapongeza wataalam na viongozi wote waliosimamia mradi huo.

 Aidha Mhe.Sendiga amesema kuwa Mkoa wa Manyara umepokea fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya uboreshaji wa huduma za maji,umeme,barabara pamoja na vituo vya afya katika halmashauri zote zilizopo Mkoa wa Manyara.

 Vilevile Mhe.Queen Sendiga amewataarifu wananchi kuwa Mkoa wa Manyara ni miongoni mwa Mikoa ya kimkakati katika uwekezaji katika sekta ya madini,kilimo na utalii ambapo amewaelezea kuwa Mkoa wa Manyara utafanya uzinduzi wa jarida maalum la uwekezaji terehe 10/10/2023.

Sambamba na hayo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga  amefanya ukaguzi wa ujenzi wa shule maalum ya Sekondari michepuo ya Sayansi kwa  wasichana ya Mkoa wa Manyara.Katika ukaguzi wake ameonyeshwa michoro ya majengo  katika ujenzi wa shule hiyo. Amefanya ukaguzi wa miundo mbinu ya maji ambayo itasaidia kutatua kero ya maji kwa wanakijiji wa Kiongozi.

 Pia ujenzi wa shule hiyo ni fursa kwa wakazi wa Kijiji cha Kiongozi katika ajira ambapo amesisitiza vijana katika kijiji hicho wapewe kipaumbele, wanawake wajasiriamali watumie vizuri fursa hiyo.Na ameomba eneo kwa Mwenyekiti wa kijiji kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi.

Matangazo

  • Tangazo kwa waliopimiwa na kurasimishiwa viwanja - Sawe na Nangara December 25, 2022
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza - 2023 December 14, 2022
  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO KWA VIJANA, WANAWAKE NA WATU WENYE ULEMAVU November 09, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI NGAZI YA TATU July 27, 2022
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Katibu Tawala Wilaya ya Babati Bw. Matipula amesisitiza juu ya upimaji wa Afya Mkoani Manyara.

    December 01, 2023
  • Mhe.Sendiga amesuluhisha mgogoro wa Ardhi Dudumera Mkoani Manyara.

    November 29, 2023
  • Mhe.Queen Sendiga amefanya mkutano na Waandishi wa Habari katika Kampeni ya Tumewasikia,Tumewafikia Mkoani Manyara.

    November 22, 2023
  • Mhe. Sendiga amefanya ziara katika Kata ya Bonga Mkoani Manyara.

    November 21, 2023
  • Tazama zaidi

Video

Halmashauri ya Mji wa Babati kuelekea miaka 61 ya Uhuru
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati