Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe.Emmanuela Kaganda amefanya ziara ya kutembelea Viongozi wa Dini na Viongozi mbalimbali ili kuwaomba Viongozi hao kuwahamasisha waumini kujitokeza kuboresha na kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Jimbo la Babati Mjini Mkoani Manyara.
Pia Mhe.Kaganda ametoa wito kwa Mama lishe na Maafisa usafirishaji (bodaboda)kujitokeza kujiandikisha katika zoezi hilo ili kupata haki ya msingi ya kupiga kura ifikapo mwaka 2025 na ameongeza kuwa makundi hayo ni muhimu sana.
Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi imetarajia kuandikisha Wapiga Kura wapya Takribani 157,958 kwa Mkoa wa Manyara kati ya Wapiga Kura wapya 5,586,433 wanaotarajiwa kuandikishwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa Nchi nzima.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati