• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango Miji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi
      • Usafi na Mazingira
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Utoaji wa Leseni ya Biashara
    • Utoaji wa Leseni za Vileo
    • Utoaji wa Kibali cha Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

Maelekezo ya utekelezaji wa Mtaala - Kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia

Imechapishwa: February 3rd, 2022

Na Nyeneu, P. R 

OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) imefanya ufuatiliaji ili kubaini namna utekelezaji wa mitaala unavyofanyika. Ufuatiliaji umeonyesha kuwa utekelezaji wa mitaala nchini kuanzia ngazi ya elimu ya awali hadi kidato cha sita umekuwa na tofauti kubwa katika ufundishaji na ujifunzaji wa maudhui yaliyokusudiwa kwa mwaka wa masomo husika. Baada ya tathmini; Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) wakaamua kuandaa mwongozo na kalenda ya utekelezaji mitaala katika ngazi za Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari. Mwongozo huu na kalenda ya utekelezaji wa mitaala umefanyiwa majaribio na kujiridhisha kuwa utasaidia kuwa dira ya ufundishaji na ujifunzaji nchi nzima.

Kalenda  hii itasaidia katika kuleta ulinganifu wa kile kinachofundishwa  kwa muda uliopangwa kwa shule zote nchini. Kalenda hii ina vipengele sita (6) ambavyo ni umahiri mkuu (mada kuu), umahiri mahususi (mada ndogo), idadi ya vipindi, mwezi, wiki na tarehe. Vipingele hivi vitamsaidia mwalimu wa somo kupanga muda wa kufundisha umahiri uliokusudiwa kwa muda muafaka. Kalenda hii itatumiwa na walimu kuandaa Azimio la Kazi pamoja na kutekeleza ujifunzaji na ufundishaji darasani kwa muda muafaka. Wasimamizi wa Elimu wakiwemo wathibiti ubora na maafisa Elimu katika ngazi ya Shule, Kata, Wilaya, Mkoa na Wizara wote watatumia kalenda hii katika kubaini umahiri wa mwalimu katika kutekeleza wajibu wake ipasavyo.

Halmashauri ya mji wa Babati kupitia Idara ya Elimu Msingi na Sekondari na Ofisi ya Mthibiti ubora wa Shule kwa kushirikiana na Ofisi ya Katibu wa Tume ya Utumishi ya Walimu (TSC) Wilaya imeendelea kutoa mafunzo katika awamu tofauti tofauti ambapo awamu ya kwanza ilikuwa ni mafunzo kwa Maafisa Elimu Kata, Maafisa wengine, Walimu wakuu na Wakuu wa Shule. Awamu ya pili ni mafunzo kwa walimu wote katika Halmashauri ambapo mafunzo ya awamu ya pili yameanza tarehe 03 Februari 2022 na kuhitimishwa tarehe 04 Februari 2022.


Imeandaliwa na Nyeneu, P. R kwa msaada wa kalenda ya utekelezaji wa Mtaala wa Elimu 2022 kutoka OR-TAMISEMI na WyEST

Matangazo

  • Tangazo kwa waliopimiwa na kurasimishiwa viwanja - Sawe na Nangara December 25, 2022
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza - 2023 December 14, 2022
  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO KWA VIJANA, WANAWAKE NA WATU WENYE ULEMAVU November 09, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI NGAZI YA TATU July 27, 2022
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Mhe.Queen Sendiga amefanya kikao na madereva wa bodaboda,bajaji.machinga na mama lishe Mkoani Manyara.

    September 20, 2023
  • Mhe.Queen Sendiga ameweka jiwe la msingi katika shule ya mpya ya Awali na Msingi

    September 15, 2023
  • Mhe. Joyce Ndalichako amekagua maandalizi ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Mkoani Manyara.

    August 28, 2023
  • Bi.Pendo Mangali amezindua ( PJT-MMMAM) ngazi ya Halmashauri ya Mji wa Babati

    August 22, 2023
  • Tazama zaidi

Video

Halmashauri ya Mji wa Babati kuelekea miaka 61 ya Uhuru
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati