Bw.Osmond Komba
Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
KITENGO CHA UKAGUZI WA NDANI.
1.Utangulizi.
Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya fedha ya serikali za mitaa ya mwaka 1982 kifungu no.48 ambacho ilitaka kila Halmashauri kuajiri mkaguzi wa ndani ambaye atafanya kazi karibu na wakuu wa Idara na vitengo na ataripoti kwa Afisa Masuhuli.
2.Watumishi wa kitengo cha Ukaguzi wa Ndani.
Kitengo cha ukaguzi wa ndani kina watumishi 02 kati ya 05 wanaohitajika.Upungufu ni watumishi 03.
3. Majukumu ya Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
i. Kuandaa mpango wa ukaguzi wa mwaka
ii. Kuhakikisha mpango wa ukaguzi unapitishwa na kamati ya ukaguzi
iii. Kuandaa program za ukaguzi kwa kila kaguzi inayofanyika
iv. Kupitia na kubaini kama mifumo ya uthibiti wa ndani unafanyakazi ipasavyo
v. Kuandaa na kutunza “current file’’kwa kila kaguzi inayofanyika
vi. Kuandaa taarifa kwa kila kaguzi inayokamilika na kuiwasilisha kwa Afisa masuhuli
vii. Kuandaa taarifa kwa kila kaguzi inayokamilika na kuiwasilisha kwa Afisa Masuhuli na Kamati ya Ukaguzi.
viii. Kutunza siri za kaguzi zinazofanyika
ix. Kuhakiki na kufunga hoja
4. Mafanikio.
• Kitengo cha ukaguzi wa ndani kimeweza kufanikiwa kutoa mafunzo na maelekezo mbalimbali kwa menejimenti nzima na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Babati,mfano uthibiti wa ndani na udhibiti wa viashiria vya vihatarishi kwenye idara mbalimbali.
• Watumishi wa kitengo cha ukaguzi wa ndani wamefanikiwa kupata mafunzo elekezi mbalimbali kuhusu utendaji kazi.
• Kitengo cha ukaguzi wa ndani kimefanikiwa kutoa ushauri mbalimbali na kufunga hoja ambazo zilikuwa na majibu sahihi na ya kutosheleza
5.Changamoto.
i. Ukosefu wa rasilimali watu,kwani Kitengo kina idadi ya watumishi 02,badala ya 05 wanaohitajika ili kutekeleza majukumu na mpango kazi wa kitengo cha ukaguzi wa ndani
ii. Ukosefu wa usafiri wa uhakika ili kuweza kukagua miradi mbalimbali kwa wakati
iii. Bajeti ndogo ya Kitengo cha ukaguzi wa ndani,ambayo inakwamisha utekelezaji wa shughuli za ukaguzi wa ndani.
6.Utatuzi wa changamoto
• Kuendelea kuomba kuongezewa watumishi toka idara ya utumishi
• Kuendelea kuomba usafiri toka idara ambazo zina gari ili kuweza kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati