Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano
Kitengo cha (TEHAMA) kimeanzishwa mwaka 2013 ambacho ni muunganiko wa Kitengo cha IT na Habari na Uhusiano. Kitengo hiki kinaongozwa na Sera ya TEHAMA (2003), na Sera ya Utangazaji Habari (2004). Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza kuwa:-
( 1) Bila ya kuathiri sheria ya nchi, na kutafuta,kupata na kueneza au kusambaza habari na mawazo kupitia chombo cha habari chochote bila ya kujali mipaka ya taifa pia anayohaki na uhuru wa kutoingiliwa na mawasiliano.
(2) Kila raia ana haki ya kupashwa habari wakati wote kuhusu matukio mbalimbali ya nchini na duniani kote yenye umuhimu kwa maisha na shughuli za wananchi , pia kwa masuala yenye umuhimu kwa jamii.
2.0 Majukumu ya Kitengo
Majukumu ya kitengo cha TEHAMA ni kama ifuatavyo:-
• Kuweka mahusiano bora baina ya Halmashauri pamoja na Umma na wadau mbalimbali pamoja na kutoa elimu kwa Umma.
• Kuandaa machapisho mbalimbali ya Halmashauri.
• Kuratibu masuala ya kiitifaki ikiwemo kupokea wageni.
• Usimamizi wa Mifumo ya Kompyuta(System Administration)
• Usimamizi wa Mtandao wa Kompyuta pamoja na vifaa vyake (Network and Hardware Adminstration).
• Usimamizi wa Benki Ya Takwimu (Database Administration)
• Usimamizi wa tovuti na barua pepe (website administration & emails).
• Kutekeleza sera ya TEHAMA na Serikali Mtandao.
• Kuandaa mahitaji katika Ununuzi wa vifaa vya TEHAMA.
• Kuandaa matukio ya mwezi na kuyawasilisha kwa Katibu Tawala kila Ijumaa ya mwisho wa mwezi.
Hivyo basi Lengo kuu la kitengo hiki ni kuhakikisha miundombinu ya TEHAMA katika Halmashauri inakuwa bora na salama katika utoaji wa huduma(taarifa).
3.0 Malengo ya Kitengo kwa Mwaka wa fedha 2016/2017
Kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Kitengo kilijiwekea malengo yafuatayo:-
• Kuweka usalama wa hifadhi data.
• Kutoa huduma za hifadhi data kwa watumiaji.
• Kusimamia maboresho ya programu za kompyuta kwa wakati.
• Kusakinisha, kusanidi na kuboresha programu za kuzuia virusi vya kompyuta. (Install, configure and update antivirus software).
• Kuelimisha watumiaji masuala mbalimbali yanayohusu usalama, hatari na udhaifu katika mifumo ya TEHAMA.
• Kukagua mifumo ya TEHAMA mara kwa mara.
• Kuweka viwango vya usalama na udhibiti katika mifumo ya TEHAMA kwa watumiaji.
• Kusanifu, kusakinisha na kusanidi miundombinu ya ndani na nje ya mtandao wa kompyuta (Desing, install and configure LAN and WAN infrastructure).
• Kufanya majaribio ya vifaa vya mtandao wa kompyuta.
• Kushauri kitaalam katika manunuzi ya vifaa bora na vya kudumu vinavyohusu TEHAMA.
• Kutengeneza vifaa vyote vya TEHAMA vinapoharibika au kutofanyakazi iliyokusudiwa kwa kupitia kwa fundi sanifu wa Kompyuta.
• Kusimamia mifumo ya kompyuta hasa mifumo ya Mapato na Mashine za Kukusanyia Mapato (Point Of Sales - POS).
• Kuboresha miundombinu ya TEHAMA ifikapo 30, Juni 2017.
• Kuimarisha ufanisi wa ufanyaji kazi wa kompyuta kwa kufanya matengenezo ya mara kwa mara ifikapo Juni 30, 2017.
• Kuwaelekeza watumiaji namna sahihi ya kutumia kompyuta ili ziweze kudumu kwa muda mrefu ifikapo Juni 30, 2017.
• Kuongeza mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato na kufikia angalau 30 ifikapo June 30, 2017.
• Kuboresha upatikanaji wa taarifa sahihi na haraka zenye ufanisi kwa kutumia tovuti na barua pepe za serikali kwa kushirikiana na Wakuu wa Idara/Vitengo mbalimbali vya Halmashauri ya Mji Babati ifikapo Juni 30, 2017.
4.0 Watumishi na Vitendea kazi
i)Watumishi
Jedwali hapo chini linaonesha mahitaji na hali halisi ya watumishi katika Kitengo cha TEHAMA kwa sasa.
Na |
Kada |
Mahitaji |
Waliopo |
Mapungufu |
1
|
Mchambuzi wa mifumo ya Kompyuta (Afisa TEHAMA).
|
2 |
2 |
0 |
2
|
Fundi sanifu wa Kompyuta (Computer Technician)
|
2 |
0 |
2 |
3
|
Afisa Habari
|
1 |
0 |
1 |
4
|
Afisa Uhusiano
|
1 |
0 |
1 |
|
Jumla |
6 |
2 |
4 |
Pamoja na upungufu wa Mtumishi huyo uliopo, kitengo kimeweza kutekeleza majukumu yake. Pia kama kungekuwa na vitendea kazi vya kutosha kitengo cha TEHAMA kingeweza kutekeleza majukumu yote ipasavyo.
ii).Vitendea Kazi
Vifaa vilivyopo havitoshi na hivyo vinaathiri sana utekelezaji wa majukumu, kitengo kimeweka katika mpango wa bajeti ya 2017/2018 kununua vifaa vya ofisi na vitendea kazi.
5.0 UTEKELEZAJI NA USIMAMIZI WA MIRADI
Kitengo kinaendelea na jukumu lake la kusimamia na kutekeleza miradi ya Miundombinu ya Ndani ya Kompyuta (LAN).
6.0 MAFANIKIO, CHANGAMOTO NA MIKAKATI
i) Mafanikio
Kuwezesha kutoa taarifa sahihi na za haraka za kifedha za ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mifumo ya mapato (LGRCIS) na matumizi (EPICOR ).
Kutoa risiti na nyaraka mbalimbali za kifedha zinapohitajika.
Kufuatilia na kuangalia mapato yaliyokusanywa kwa kutumia POS zilizogawanywa kwa watendaji.
Kuthibiti au kupunguza makosa yaliyojitokeza katika ukusanyaji wa kawaida kwa kutumia vitabu .
Kuwawezesha walipa bili kulipa na kuangalia bili zao za huduma mbalimbali kama vile leseni za biashara, kwa kutumia simu za kiganjani iliyounganishwa na NMB mobile kwa kuwa LGRCIS (Local Government Revenue Collection Information System) imeunganishwa na CCS (Cash Collection System)..
Kuongezeka kwa ustadi wa watumiaji wa kompyuta na mifumo ya kompyuta baada ya kutoa maelekezo sahihi ya utumiaji wa kompyuta kwa watumiaji hao.
Kupungua kwa changamoto za upotevu wa taarifa miongoni wa watumiaji wa kompyuta.
ii)Changamoto .
• Ufinyu wa bajeti, kitengo cha TEHAMA kinategemea sana mapato ya ndani na hivyo kuathiri utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kitengo kwa kuwa fedha hizo hazitoshelezi.
• Ukosefu wa fedha ya kuhudhuria mafunzo ya TEHAMA kikamilifu endapo kama mafunzo yanahitaji Halmashuri kulipia, hii ni kutokana na ukosefu wa fedha.
• Halmashauri haina Computer Server ambayo ingeweza kuhifadhi baadhi ya taarifa muhimu.
• Ukosefu wa Internet husababisha taarifa mbalimbali zinazotumwa nje ya Halmashauri kuchelewa hii ni kutokana na kutolipiwa bill ya intaneti kitu kinachopelekea Kampuni ya TTCL kukata intaneti.
iii)Mikakati ya kupambana na Changamoto.
• Kuongeza jitihada za kubuni njia mbalimbali za kukusanya mapato ili kuwa na fedha za kutatua changamoto.
• Kuomba nyaraka kwa maafisa TEHAMA wenzetu waliohudhuria mafunzo mbalimbali na kusoma ili kutatua changamoto za mifumo.
• Kuomba msaada wa kitaalam katika kitengo cha TEHAMA kilichopo ofisi ya TAMISEMI.
• Kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kulipa ushuru na matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato (POS).
• Kuendelea kuongeza mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato (POS).
• Kuendelea kushirikiana na idara na vitengo vinavyotumia kompyuta ili kupata taarifa kama kutakuwa na matatizo ya kiufundi ili yaweze kutatuliwa mara moja.
• Ili kupunguza tatizo la internet , tunaendelea na mchakato wa kuunganisha Mkonga wa Taifa kwa kufunga wired na wireless router kupitia kampuni ya TTCL (Tanzania Telecomunication Limited) unaendelea, ambayo itawezesha kutoa huduma ya internet kwa gharama nafuu katika Halmashauri ya Mji Babati.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati