Bi.Rena Urio
Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi
IDARA YA MIFUGO NA UVUVI
1.0. Utangulizi
Sekta ya Mifugo ina nafasi kubwa katika kujenga uchumi imara wa Taifa, kuongeza kipato kwa watanzania wanaotegemea mifugo na kutoa fursa ya ajira na kuhifadhi rasilimali za Taifa. Hii ni kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Mifugo ya mwaka 2006. Dira ya sekta ya Mifugo kama ilivyokubaliwa na wadau wa sekta mwezi Aprili 2001 inatamka “Kuwe na Sekta ya Mifugo ambayo ifikapo mwaka 2025 kwa sehemu kubwa, itakuwa na ufugaji wa kisasa na endelevu, yenye mifugo bora, yenye uzalishaji mzuri, inayoendeshwa kibiashara na yenye kuboresha lishe ya Mtanzania, kuinua kipato cha mfugaji na Taifa na kuhifadhi mazingira”.
Sera ya Taifa ya Uvuvi ya mwaka 1997 inalenga kuweka mazingira mazuri ya kuhifadhi na kuendeleza rasilimali za uvuvi. Tamko hili linalenga katika ukuzaji wa matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi ili kuongeza chakula, mapato, ajira na kuweka usimamizi madhubuti wa mazingira ya majini ili kudumisha maendeleo ya jamii.
2.0. Majukumu ya Idara ya Mifugo na Uvuvi
Idara ya Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Mji wa Babati inatekeleza majukumu yake kwa wafugaji kama inavyoonesha hapa chini:-
i. Kufanya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa wafugaji katika kata zote za Halmashauri.
ii. Kukagua nyama na usafi wa machinjio mara kwa mara.
iii. Kutibu magonjwa ya mifugo na kushauri wafugaji jinsi ya kukinga mifugo dhidi ya magonjwa.
iv. Kutembelea wafugaji mara kwa mara na kuwapa ushauri fasaha wa kitaalam.
v. Kukusanya takwimu zote za maendeleo ya mifugo katika eneo la Halmashauri.
vi. Kufanya uhamilishaji (Artificial Insemination) na uzalishaji (breeding) wa mifugo kwa jumla.
vii. Kushauri wafugaji kuhusu mbinu bora za kuzalisha maziwa na utunzaji wa ndama.
viii. Kushauri wafugaji umuhimu wa kupunguza mifugo yao kulingana na maeneo/malisho.
ix. Kutoa taarifa za milipuko ya magonjwa na viumbe waharibifu.
x. Kuandaa ratiba cha chanjo na mipango ya uchanjaji
xi. Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wakala wa pembejeo muhimu za mifugo.
xii. Kuwa kiungo kati ya vikundi vya wafugaji na watafiti.
xiii. Kukagua na kuidhinisha vibali vya usafirishaji wa mifugo.
xiv. Kuendeleza uvunaji endelevu wa samaki na viumbe wengine wa baharini, maziwa, mito, mabwawa na malambo
xv. Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu uvuvi bora, utengenezaji na uhifadhi bora wa samaki na mazao ya uvuvi, biashara na masoko ya samaki pamoja na ufugaji wa samaki na viumbe wengine wa majini
xvi. Kutoa leseni za uvuvi na kuendesha mafunzo ya taaluma ya uvuvi
xvii. Kusimamia na kutekeleza sheria za uvuvi (kwa mfano kuzuia uvuvi haramu)
xviii. Kuratibu shughuli za utafiti wa uvuvi
xix. Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali ya uvuvi
xx. Kukagua ubora wa samaki na mazao ya uvuvi na kuweka viwango vya kitaifa.
a) Shughuli za kawaida.
• Kukagua nyama
• Kutoa kinga na tiba kwa mifugo
• Kutoa elimu juu ya Ukaushaji wa ngozi
• Uogeshaji wa mifugo
• Kutoa huduma mbalimbali kama kukata kwato, kukata mikia, kuhasi, kukata midomo.
• Kusimamia, kulinda na kuhifadhi rasilimali za ziwa Babati kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
• Kudhibiti uvuvi haramu
• Kutoa elimu ya uvuvi endelevu juu ya matumizi endelevu ya ziwa Babati
• Kutoa elimu ya ufugaji wa samaki bwawani
b) Miradi ya maendeleo.
• Ukarabati wa machinjio ya Halmashauri ya Mji
• Ujenzi wa ofisi ya uvuvi mtaa wa Nangara ziwani
• Kufanya utafiti katika ziwa Babati
• Kujenga uzio, choo na maji katika mnada wa Gendi
4.0. Hali ya watumishi
Idara ya Mifugo na Uvuvi inahitaji watumishi 18 ambapo kwa sasa wapo watumishi 14 hivyo kuwa na upungufu wa watumishi 4.
5.0. Vitendeakazi
Idara ya Mifugo na Uvuvi ina pikipiki 8 na kuwa na upungufu wa pikipiki 5, laptop 3 pungufu ni laptop 3, desktop mbovu 2 pungufu desktop 2, printer 1 pungufu 2.
6.0. Changamoto za idara
Ukosefu wa fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli za mifugo ikiwemo miradi, vitendea kazi, uvuvi haramu.
7.0. Utatuzi wa changamoto
Kuendelea kihimiza Halmashauri kutoa fedha za kutosha ili kuweza kutekeleza shughuli za idara.
Barabara ya Babati - Singida
Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati
Nukushi: +255-027-2510095
Simu: +255-027-2510095
Barua pepe: td@babatitc.go.tz
Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati