• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango Miji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi
      • Usafi na Mazingira
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Utoaji wa Leseni ya Biashara
    • Utoaji wa Leseni za Vileo
    • Utoaji wa Kibali cha Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

Elimu Sekondari



MUUNDO WA IDARA YA ELIMU SEKONDARI
UTANGULIZI
Halmashauri ya Mji wa Babati ina jumla ya Shule za Sekondari 18 kati ya hizo Shule 12 ni za Serikali na Shule 06 ni za Binafsi. Shule za serikali zina jumla ya Wanafunzi 6177 kati yao wavulana 2655 na wasichana 3522 na shule za Binafsi zina Jumla ya 2231 kati yao wavulana ni 1132 na wasichana ni 1100. Halmashauri ina jumla ya walimu 375 katika shule za sekondari za serikali.
 
MAJUKUMU YA MKUU WA IDARA YA ELIMU SEKONDARI WA HALMASHAURI
Ni Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari wa Halmashauri. Majukumu yake ni pamoja na:-
  • Kuiwakilisha Wizara katika halmashauri kuhusu masuala ya elimu sekondari .
  • Kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na kanuni zinazoongoza utoaji wa elimu ya sekondari
  • Kusimamia upanuzi wa elimu ya sekondari katika halmashauri
  • Kusimamia haki na maslahi ya walimu na watumishi wengine wa ngazi ya elimu ya sekondari katika halmashauri
  • Kusimamia na kudhibiti akaunti ya elimu ya sekondari na kuhakikisha kuwa fedha za elimu ya sekondari zinatumika kama ilivyokusudiwa
  • Kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu ya sekondari
  • Kufuatilia na kutathmini maendeleo ya elimu ya sekondari katika halmashauri
  • Khakikisha kuwa shule zote za sekondari katika halmashauri zinainua ubora wa mazingira ya kujifunzia na kujifundishia ikiwa ni pamoja na utunzaji wa madarasa, nyumba za walimu, maabara, maktaba na vyoo
  • Kusimamia tathmini  ya wazi ya utendaji kazi (Open Performance Review and Appraisal System -OPRAS)  kwa walimu na watumishi wa sekondari
  • Kuhimiza udhibiti wa nidhamu ya walimu, watumishi na wanafunzi wa shule  za sekondari katika halmashauri
  • Kumshauri mkurugenzi wa halmashauri kuhusu masuala yote ya elimu ya sekondari 
  • Kufanya kazi nyingine kama itakavyoelekezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri

MAJUKUMU YA AFISA ELIMU TAALUMA SEKONDARI WA HALMASHAURI
Afisa Elimu Taaluma wa Sekondari anatekeleza majukumu yafuatayo katika Halmashauri:-
  • Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa shule za sekondari.
  •  Kubuni mipango ya mitihani ya elimu ya sekondari na kusimamia utekelezaji wake

  • Kuhakikisha kuwa walimu na watumishi wengine wa shuke za sekondari wanafanyiwa tathmini ya wazi ya utendaji kazi (Open Performance Review and Appraisal System-OPRAS)

  • Kubuni na kuratibu mipango ya mafunzo kazini kwa walimu na watumishi wengine wa shule za sekondari.

  • Kuratibu mashindano ya michezo na Taaluma ya shule za sekondari katika Halmashauri (UMISSETA).

  • Kuratibu utoaji wa huduma mbalimbali kwa wanafunzi wa shule za sekondari katika Halmashauri

  • Kufanya kazi nyingine atakazopewa na Mkurugenzi wa Halmashauri au Afisa Elimu wa Elimu ya Sekondari wa Halmashauri.


MAJUKUMU YA AFISA ELIMU VIFAA NA TAKWIMU WA SEKONDARI WA HALMASHAURI
Majukumu ya Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Sekondari wa Halmashauri ni haya yafuatayo:-
  • Kuratibu, kukusanya na kuchambua takwimu za elimu ya Sekondari katika Halmashauri.
  • Kusimamia na kufuatilia ukarabati, upanuzi na ujenzi wa shule za sekondari.
  • Kufanya makisio ya mahitaji ya walimu kimadaraja na kimasomo.
  • Kuagiza na kusambaza vifaa vya shule kulingana na mahitaji ya Halmashauri na shule.
  • Kufuatilia mapato na matumizi ya fedha katika shule za sekondari.
  • Kufuatilia utekelezaji wa huduma mbalimbali kwa wanafunzi
  • Kufanya kazi nyingine kama itakavyoelekezwa na Afisa Elimu wa Sekondari wa Halmashauri au Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri. 

MAJUKUMU YA AFISA ELIMU KATA
Majukumu ya Afisa Elimu Kata yamegawanyika katika majukumu ya kiutawala na majukumu ya kitaaluma kama inavyofafanuliwa hapa chini:-

a) Majukumu ya Kiutawala
  • Kusimamia utekelezaji wa sera, kanuni na miongozo ya usimamizi na uendeshaji wa elimu katika kata.
  • Kuwa mshauri wa Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) katika mambo yanayohusu 
  • Elimu ya Sekondari katika Kata.
  • Kushirikiana na Kamati ya maendeleo ya Kata na Afisa Elimu wa Sekondari kuchagua 
  • maeneo yanayopendekezwa kujenga shule mpya na kuendeleza ujenzi wake.
  • Kufanya ufuatiliaji wa shughuli za ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule.
  • Kuhamasisha jamii kuchangia fedha na nguvukazi katika ujenzi wa shule mpya na kuimarisha miundombinu ya shule zilizopo.
  • Kupokea na kupitisha Mpango Shirikishi wa maendeleo ya shule, bajeti na taarifa za utekelezaji
  • Kushirikiana na uongozi wa Kata na vijiji kuhakikisha wanafunzi wanaojiunga na Kidato cha kwanza, wanaandikishwa, wanahudhuria na kumaliza elimu ya sekondari bila vikwazo vyovyote.
  • Kuratibu upatikanaji wa takwimu za shule za sekondari kwa kushirikiana na Afisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Sekondari wa Halmashauri.
b) Majukumu ya Kitaaluma
  • Majukumu ya kitaaluma ya Afisa Elimu Kata ni pamoja na:-
  • Kushirikiana na uongozi wa shule za sekondari katika kupanga na kusimamia mbinu mpya za kusimamia taaluma shuleni.
  • Kushirikiana na menejimenti za Shule za Sekondari katika kuweka mikakati ya kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji shuleni.
  • Afisa Elimu Kata ni mkaguzi wa ndani. Hutoa ushauri wa utoaji wa taaluma katika shule za sekondari na kuwasilisha taarifa kwa Afisa 
  • Elimu Sekondari wa Halmashauri. Katika utekelezaji wa jukumu hili atawasiliana na Mkuu wa Shule kupata kumbukumbu zote muhimu.
MAJUKUMU YA BODI YA SHULE
Kila shule ya Sekondari katika Halmashauri inapaswa kuwa na Bodi ya shule. Bodi za shule zimeanzishwa kwa mujibu wa kifungu
 cha 39 cha Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 kikisomwa pamoja na kanuni za elimu. Pamoja na mambo mengine. Bodi ya Shule itakuwa na majukumu ya kupitia na kuelekeza Wakuu wa Shule kuhusu masuala ya fedha za shule.

Katika kutekeleza majukumu yake, bodi inatakiwa:-
  • Kupitia, kujadili na kuidhinisha bajeti ya shule
  • Kupitia na kujadili ripoti za fedha za robo mwaka na za mwisho wa mwaka.
  • Kuteua kamati ndogo ya kusimamia mfuko wa maduhuli, manunuzi na  ujenzi
  • Kujadili na kupitisha maombi ya manunuzi ya bidhaa, huduma, ujenzi, vifaa na vifaa kufundishia na kujifunzia.
 MAJUKUMU YA MKUU WA SHULE
  • Kusimamia utekelezaji wa mtaala
  • Kuwa Mkaguzi wa ndani na wa awali wa ufundishaji wa walimu.
  • Kupokea na kusajili wanafunzi wapya.
  • Kusimamia mali zote za shule.
  • Kutafsiri,kusimamia na kutekeleza Sera, sharia, ya Elimu, Kanuni na nyaraka mbalimbali za elimu.
  • Kuandaa, kusambaza na kutumia taarifa na takwimu za shule kwa wakati na zikiwa sahihi.
  • Kukusanya na kusimamia mapato na matumizi ya fedha za shule kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za nchi.
  • Kuandaa, kusimamia na kuendesha mafunzo ya ndani kwa walimu ikiwa ni pamoja na kutoa “orientation” kwa walimu wapya.
  • Kusimamia ustawi wa walimu na wanafunzi ili kila mmoja awajibike na apate haki zake zote kadri inavyowezekana.
  • Kuandaa wa jumla wa shule na mpango wa maendeleo, mpango wa kazi na kuwasilisha ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya kata na Halmashauri.
  • Kuwa kiungo kati ya shule na jamii pana.
  • Kuwa Katibu wa vikao vya Bodi ya Shule na kuhakikisha inakuwa hai wakati wote. Bodi huwa na vikao vya kawaida
  •  visivyopungua vine. Bodi ndicho chombo kikuu cha kumsaidia Mkuu wa Shule kuendesha shule.
  • Kufundisha masomo aliyosomea ili kuwa mfano (model) na kuimarisha ualimu wa Mkuu wa Shule.
  • Kusimamia na kudumisha nidhamu kwa wanafunzi na maadili kwa walimu ili kurejesha heshima ya ualimu.
  • Kuboresha mazingira ya shule ikiwa ni pamoja na kuyajanisha na kutengeneza viunga.
  • Kusimamia ukarabati wa miundombinu ya shule yakiwemo majengo na madawati ili yawe katika hali bora wakati wote.

HALI YA TAALUMA
MIKAKATI YA KUBORESHA TAALUMA KWA MWAKA 2021
CHANGAMOTO
UTATUZI WA CHANGAMOTO


Matangazo

  • Tangazo kwa waliopimiwa na kurasimishiwa viwanja - Sawe na Nangara December 25, 2022
  • Wanafunzi Waliochaguliwa Kidato cha Kwanza - 2023 December 14, 2022
  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO KWA VIJANA, WANAWAKE NA WATU WENYE ULEMAVU November 09, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE MAFUNZO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI NGAZI YA TATU July 27, 2022
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Waziri Kairuki atoa angalizo utekelezaji mradi wa BOOST

    December 13, 2022
  • Mhe. Jenista Mhagama awasisitiza watendaji wa ofisi yake kuwa na kauli nzuri na kutoa huduma bora kwa wananchi na watumishi wanaowahudumia

    December 04, 2022
  • Maagizo ya DC Twange kwa Watumishi wa Umma na Wafanyabiashara kuhusiana na utoaji wa risiti za EFD

    December 02, 2022
  • Rais Samia azindua miradi miwili mikubwa iliyogharimu Mabilioni ya fedha Mjini Babati

    November 22, 2022
  • Tazama zaidi

Video

Halmashauri ya Mji wa Babati kuelekea miaka 61 ya Uhuru
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati