• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango Miji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumisha
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

Uwezeshwaji wa Wananchi Kiuchumi.

Imechapishwa: September 24th, 2020

Idara ya maendeleo ya jamii kupitia kitengo cha mikopo katika halmashauri ya mji wa Babati leo tarehe 23. 9. 2020 imeendelea kutoa mafunzo kwa vikundi vinavyotarajiwa kupata mikopo. Mafunzo hayo yanahusiana na elimu ya ujasiriamali kwa makundi matatu, ambayo ni wanawake, vijana na walemavu. Mikopo hii inatokana na asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani ya halmashauri. Katika kutekeleza hili idara imeweza kutoa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wasafirishaji (bodaboda).

Wakizungumza na waombaji mikopo, katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, watumishi wa idara hiyo wamezidi kusisitiza sifa na kanuni zinazowataka waombaji wa mikopo kutekeleza. Ambapo idara inamtaka kila muombaji, awe ana wadhamini, awe mmoja kati ya makundi tajwa (wanawake, vijana na walemavu), awe na katiba, awe amewasilisha andiko la mradi(Proposal), kurejesha mkopo baada ya mwaka mmoja na kusisitiza kuwa ni jukumu la mdhamini kulipa mkopo ikiwa mkopaji atashindwa kulipa kwa wakati (ndani ya mwaka mmoja).

Aidha, katika mafunzo hayo watumishi hao wameeleza lengo la serikali katika ugawaji wa mikopo. Serikali imelenga kuwezesha wananchi kiuchumi, kutoa ajira kwa makundi tajwa, kupunguza watu tegemezi na kukuza pato la taifa kwa ujumla inayotazamiwa kulipwa na wakopaji kulipia biashara zao. Baada ya serikali kuona baadhi ya wananchi wanakimbia na mikopo hapo awali ndipo ilipoamua kukata shauri na kuweka utaratibu wa kufatilia utendaji kazi wa pesa za mikopo kwa wajasiriamali. Na pia kutoa shamba darasa, namna ya kujiepusha na hasara katika biashara kwa kuwa na biashara mbadala.

Sambamba na utoaji wa mikopo pia idara kupitia Ofisi mbalimbali imeweza kutoa elimu mbalimbali kwa waombaji mikopo, ambapo elimu hiyo itawasaidia wachukua mikopo kupiga hatua. Elimu hiyo ni elimu ya ujasiriamali, ukatili wa kijinsia, kilimo na biashara, ufugaji wa kisasa, taratibu za kitaalamu (kutunza kumbukumbu), kufuata sheria za nchi wakati wa utendaji kazi, kuelimisha na kuhamasisha kuhusu utoaji wa mikopo na kuhusu usalama barabarani. Yote haya yanaweza kumuwezesha mjasiriamali aliyechukua mkopo kupiga hatua zaidi.

(Picha: Nyeneu, P. R) Mmoja kati ya wawezeshaji walioshiriki kutoa mafunzo(Elimu) ya usalama barabarani kwa waombaji wa mikopo Mjini Babati katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji.

Watumishi wa idara hiyo (Maendeleo ya jamii na ustawi) wameeleza kuwa muitikio wa wananchi wa mji wa Babati katika kujiunga na uchukuaji wa mikopo umekua mkubwa sana ukilinganisha na hapo awali. Na hii ni kutokana na mikopo hii kutokua na riba ukilinganisha na taasisi nyingne za fedha nchini zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali.

Pia mtumishi huyo amezidi kuwaasa wananchi wa mji wa Babati kujiunga na huduma hii ya mikopo kwani ina lengo la kuwainua kiuchumi kama alivyosema “Mimi maoni yangu kwa Wanababati ni kujiunga na uchukuaji wa mikopo ili kijiendeleza zaidi. Lakini pia nisisitize kuhusu swala la uaminifu katika urejeshaji wa mikopo” kwa kumalizia hayo mtumishi huyo anazidi kusisitiza wachukua mikopo kuwa waaminifu kurejesha mikopo yao kwa wakati na bila usumbufu wa aina yoyote.

Sheria ya serikali siku zote sharti kutimizwa. Kwa kulitambua hilo halmashauri ya mji wa Babati kupitia idara ya maendeleo ya jamii katika kitengo cha mikopo, imeona si vyema kung’ang’ania asilimi kumi (10%) za mapato ya ndani ya halmashauri, bali kutoa mikopo kwa makundi tajwa kama serikali ilivyoagiza.

Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 BABATI MJI December 18, 2020
  • ORODHA YA WASIMAMIZI WA VITUO, WASIMAMIZI WASAIDIZI WA VITUO NA MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA October 20, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA September 21, 2020
  • TANGAZO KWA WALE AMBAO HAWAJAENDELEZA MAENEO YA KUJENGA VIBANDA UWANJA WA KWARAA August 15, 2020
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Baraza la Mtihani (NECTA) latangaza matokeo - CSEE, FTNA, QT na SFNA

    January 15, 2021
  • TASAF yazindua mfumo mpya wa malipo kwa Walengwa

    December 18, 2020
  • Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi amshukuru Mhe. Rais Mbele ya Baraza la Madiwani Mjini Babati

    December 11, 2020
  • Karibuni watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino - DC Twange

    November 28, 2020
  • Tazama zaidi

Video

MWENGE WA UHURU 2018 KARIBU BABATI MJI.
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati