• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Barua pepe kwa wafanyikazi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Babati Town Council
Babati Town Council

Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Babati

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na utumishi
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango Miji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Madini
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumisha
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Huduma za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • UKIMWI
      • Maadili
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Vyombo
    • Hotuba
    • Picha
    • Video
    • Habari

TALGWU Kuhakikisha Wanawake wanaheshimika Makazini

Imechapishwa: March 8th, 2021

Na Nyeneu, P. R (Kaimu Afisa Habari)

Picha zote Na Nyeneu, P. R

Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Twange, ambaye alikuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Mkuu wa mkoa, ameyapokea kwa furaha kabisa maandamano ya wanawake Mkoa wa Manyara katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani Mkoani humo yaliyofanyika Babati Mjini, huku wakiwa wamebeba mabango kutoka taasisi mbalimbali yenye ujumbe uliosomeka “Wanawake Katika Uongozi, Chachu kufikia Dunia yenye Usawa” ikiwa ni kaulimbiu ya siku ya wanawake Duniani kwa mwaka 2021.

Aidha, mjumbe wa kamati ya utendaji ya chama Taifa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) Mkoa wa Manyara Bi. Devotha Edwin Mbonamasabu katika maazimisho ya siku ya wanawake Duniani Machi 8 2021, amesema kazi kubwa ya Chama ni kuhakikisha mustakabali wa wanawake kupitia kamati ya ushauri ya wafanyakazi wanawake unalindwa na wafanyakazi wanawake wanaheshimika makazini.

Pia, Mhe. DC aliweza kuzindua maonyesho ya wajasiriamali wadogo na wa kati yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Vinywaji ya Mati Super Brand Limited mjini Babati.

“Sisi kama Mati Super Brand Limited tumedhamini maonyesho haya ya wajasiriamali wadogo na wa kati Babati Mkoani Manyara kwaajili ya kuweza kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwainua wajasiriamali na kuweza kujenga uchumi.” Alieleza meneja Mauzo na Masoko.

Sambamba na hilo, Mkuu wa Mkoa Mhe. Joseph J Mkirikiti akiambatana na Rais wa Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Bw. Phares Magesa, Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro J Twange, Katibu Tawala Wilaya Ndg Halfan Matipula Pamoja na viongozi na wadau mbalimbali rasmi wameuzindua uwanja wa Mpira wa Kikapu Mjini Babati mara tu baada ya Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Pamoja na maonyesho ya Wajasiriamali wadogo kufikia mwisho.

Uwanja huo wa kisasa umegharimu pesa taslimu zisizopungua Shilingi Milioni 10, umejengwa kwa nguvu za wadau mbalimbali mjini Babati, ambapo wadau walijitolea kuchangia vitu, fedha na nguvu kazi.

“Mheshimiwa Mgeni Rasmi, napenda kuchukua nafasi hii kukueleza wazi kabisa, hadi uwanja huu unakamalika, wananchi wa mkoa wa Manyara hususani wa mji wa Babati wamejitolea kutoa kokoto karibia trip 16, mchanga trip 12, mawe trip 10, mifuko ya simenti 176” Alifafanua zaidi Afisa Michezo Mkoa

Vile vile akina mama wa Sokoni hawakukubali kuwa nyuma katika kuhakiksha uwanja wa Mpira wa Kikapu Unajengwa na kukamilika, ambapo wao walijitolea nyanya, vitunguu, mboga mboga pamoja na vitu vingine, pia watu wenye maduka walitoa mchele na wenye mabucha walitoa nyama ili kuhakikisha mafundi wanaweza kula.

Aidha, Uongozi wa Michezo mkoa wa Manyara umejiwekea malengo ya kujenga kiwanja kila baada ya Mwezi mmoja na pia kuhamasisha kila halmashauri mkoani humo kuiga mfano wa watu wa Mji wa Babati ili waweze kujenga viwanja kwenye halmashauri zao.

Bw. Phares Magesa katika hotuba yake amewapongeza sana wana Babati kwa moyo wao wa kujitolea katika ujenzi wa viwanja tena kwa nguvu zao wenyewe. Hii itapelekea kuwepo na viwanja vya kutoka baada yam waka mmoja. Katika kuunga mkono juhudi hizo, Bw. Magesa amekabidhi mipira miwili ya Mpira wa Kikapu kwa timu mbili za Mchezo huo.

Baada ya Mhe. Mkuu wa Mkoa kumaliza zoezi la uzinduzi wa uwanja huo, kukawa na Mashindano ya Mpira wa kikapu ambapo timu ya Tanzanite iliumana vikali na Timu ya Tarangire. Timu ya Tarangire iliweza kuichapa bila huruma timu ya Tanzanite Vikapu 103 kwa vikapu 81.

Wakati huo huo kulikuwa na mtanange mkali wa mpira wa miguu ambapo timu ya Matipa FC iliweza kutoshana nguvu na timu ya Boda Boda FC baada ya kutoka sare ya magoli 1 kwa 1.



Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 BABATI MJI December 18, 2020
  • ORODHA YA WASIMAMIZI WA VITUO, WASIMAMIZI WASAIDIZI WA VITUO NA MAKARANI WAONGOZAJI WAPIGA KURA October 20, 2020
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA September 21, 2020
  • TANGAZO KWA WALE AMBAO HAWAJAENDELEZA MAENEO YA KUJENGA VIBANDA UWANJA WA KWARAA August 15, 2020
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • Yafahamu mambo yafuatayo kuhusu Afya ya Kinywa na Meno

    March 30, 2021
  • Babati Mji waadhimisha siku ya afya ya Kinywa na Meno Duniani Mashuleni

    March 17, 2021
  • TALGWU Kuhakikisha Wanawake wanaheshimika Makazini

    March 08, 2021
  • Baraza la Mtihani (NECTA) latangaza matokeo - CSEE, FTNA, QT na SFNA

    January 15, 2021
  • Tazama zaidi

Video

Mpango Mkakati wa Halmashauri ya Mji/DC Twange atoa pongezi/Azungumzia Babati Mji kuwa Manispaa
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Idara ya Habari - Maelezo
  • Salary Slip Portal
  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Mfumo wa Maombi ya Kazi
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara
  • Halmashauri ya Mji wa Mbulu
  • Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
  • Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
  • Halmashauri ya Wilaya Mbulu

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Sanduku la Posta: P.O.Box 383 Babati

    Nukushi: +255-027-2510095

    Simu: +255-027-2510095

    Barua pepe: td@babatitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hatimiliki@2021 Haki zote zimehifadhiwa na Halmashauri ya Mji Babati